Monday, January 14, 2013

Ndizi za chakula na biashara

Umaarufu wa zao la ndizi unazidi kuenea kwa kasi zaidi kutokana na juhudi za watafiti kuingiza aina mpya za migomba kutoka Jamaica aina hizo ni ndizi ziitwazo grandnaine, williams na cavindish ambazo zimeibuka kupendwa sana na wakulima pamoja na walaji kwa sifa zake za kuzaa kwa muda mfupi, umbile zuri, utamu kwa chakula, utamu kama tunda,kuhifadhika kwa muda mrefu bila kuharibika na faida inayopatikana kwa biashara ya zao hilo. Mkungu mmoja unaweza kuwa na chani za ndizi hadi kufikia hadi 20!Hapa nchini ndizo hizo zimeenea katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Pwani, Dar Es Salaam, Lindi, Unguja, Pemba Ruvuma na Mtwara. Mjini Arusha kwa sasa mkungu kama huo ulipo pichani huuzwa kwa shilingi 30,000/= lakini shambani kwa mkulima huuzwa kati ya shilingi 15,000/= hadi 20,000/= wilayani Babati.(Picha imetumwa na Livingstone Mwedipando - ARI-Selian, Arusha)Picha inaonyesha mkungu awa ndizi aina ya Williams

No comments: