Thursday, January 3, 2013

MWAKA MPYA 2013

Wasomaji wa Banzi wa Moro. Namshukuru Mungu kwa yote aliyonijalia pamoja na changamoto zilizojitokeza mwaka 2012. Mwaka wa jana 2012 Banzi wa Moro imepata mafaniko makubwa kwa kuingiza posts 573 ukilinganisha na 476 za mwaka 2011.Angalia takwimu hizi hakika zinaeleza kitu 2006 (16);2007(16);2008(195);2009(250);2010(313);2011(476) na 2012 (573). Nashukuru kwa sasa pia kuna wapitiaji takribani 108 wa mtandao huu. Aidha wasomaji wengi wamejitokeza kutoa maoni yao,shem Bello bado anaongoza kwa hilo asante sana. Alikuwa wa kwanza mwaka 2006 aliponitahadharisha kuwa post 16 hazitoshi kwa mwaka! Nachukua fursa hii kumshukuru ndugu yangu na kaka yangu Livingstone Mwedipando kutoka ARI-Selian Arusha. Yeye ameweza kuchangia posts nyingi kwenye blog hii kwa mwaka 2012 hasa picha nyingi za utafiti na mji wa Arusha. Ile zahanati ya mimea ilitumwa na kaka Mwedipando. Nimekuwa na posts nyingi kutoka Parokia ya Vikindu pia. Blog imepata posts nyingi za harusi, Kupokea komunio ya kwanza na kipaimara zote ikiwa zimefanyika katika Parokia ya Mt. Visenti wa Paulo Vikindu. Ndugu zangu wa AFRICANA hawakukosekana kwenye Blog hii. Kila nilipopata fursa nilihakikisha kuwa wamo kwani hawa wote ni 'KIBANDA KIMOJA' (K2). Nasema asante nawakaribisha tena kwenye banzi wa Moro kwa mwaka 2013. HERI YA MWAKA MPYA! Karibuni Kisemvule msiogope sitting room kwenye mkorosho!

No comments: