Friday, January 4, 2013

Ni wachache wanaofahamu lugha ya Mashairi

Nilipokuwa shule ya msingi nilikuwa mahiri wa kutunga na kuimba mashairi niliweza kusoma mashairi katika mashindano yaliyowashindanisha wanafunzi kutoka madarasa mbalimbali. Na kwakweli niliyaelewa na hata kanuni za utunzi wake kama vile vina n.k. Siku hizi hata ile hamu ya kupitia mashairi yanayoandikwa kwenye magazeti sina. Hakuna anayehamasisha kuyapenda mashairi. Hata wale wapenzi wa lugha ya kiingereza sioni kama wako vizuri kwenye eneo hili. Mashairi yanatakiwa kuwa na tafakari ya akina na tajiri wa lugha siyo kukata na na kubandika (copy and paste).

No comments: