Monday, January 7, 2013

Vituko vitatu vya kwaya

Jana tarehe 6/1/2012 Kwaya ya Mt. Visenti wa Paulo, Parokia ya Vikindu iliwakaribisha kwaya ya Mt. Augustino kigango cha Chamazi, Parokia ya Mbagala. Wakati wa kutoa maoni yake kuhusu kwaya, Mlezi wa Kwaya ya Mt. Visenti wa Paulo, Bw. Clement Matwanga aliweka wazi vituko vitatu vya kwaya ambavyo visipodhibitiwa vinaweza kuua kwaya vituko hivyo ni:- 1)Je wana kwaya wakiwa katika kanisa lao (kwao) wanaimba kama wanavyoimba wakiwa nje ya kanisa lao? ( Ni aghalabu sana) 2) Wanaokiharibu kikundi cha kwaya mara nyingi ni walimu wa kwaya (kwa kujiona wao ni zaidi) 3) Wanaokiharibu kikundi cha kwaya mara nyingi ni wanakwaya wenyewe (hawataki mabadiliko,hawafiki mazoezini)

No comments: