Friday, January 4, 2013

Wachina wanaweza kukurefusha

Leo mchana nimepata bahati ya kuiona article moja kwenye gazeti la dailynews la tarehe 14/4/2010 iliyoandikwa 'with saw, screwdriver, China doctor gives gift of height' ( Kwa msumeno,na bisibisi daktari wa kichina natoa zawadi ya urefu-Tafsiri yangu). Dr. Bai Helong kwa miaka zaidi ya 15 amekuwa akitoa zawadi ya kuwaongezea urefu watu wapatao 3,000 wenye umri wa miaka kati ya 14 na 55 wakiwemo Wachina, Wajerumani na Wajapani.Inasemekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu hao hufanyiwa operesheni hiyo kwa sabababu tu wanachukizwa kuwa wafupi.Teknolojia hii ya kurefusha umbo ni ya siku nyingi ni kwa mara ya kwanza ilifanyika miaka ya 1950 kwa iliyokuwa Umoja wa nchi za Kisoviet baadaye China. Dkt. Bai anasema kuwa tangu mwaka 1995 hukuna operesheni iliyoshindikana.Wenzetu wanafikiri jinsi ya kutatua matatizo ya watu wanafanya utafiti na hatimaye kupata teknolojia!(source14/4/2010Dailynews)

No comments: