Wednesday, November 12, 2014

Tido Muhando-Mwandishi nguli

             Huyu ndiye Mwandishi wa habari wa Kimataifa Dunstan Tido Mhando. Mwandishi mahiri    na     mtangazaji pia. Enzi zake alipokuwa Radio Tanzania alikuwa akitangaza vizuri sana kipindi cha michezo na hasa matangazo ya moja kwa moja ya soka. Alipokuwa BBC alikuwa akitupasha habari kemkem kutoka Bara la Afrika. Amefanya mahojiano na marais mashuhuri wa Bara la Afrika akiwemo Baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere, Hayati Laurent Kabila aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Rais Paul Kagame na Rais Yoweri Mseveni. Katika mahojiano yake na Hayati Laurent Kabila ilibainika kuwa alikuwa shabiki mkuwa wa klabu ya Soka Simba ya jijini Dar, Tanzania.

No comments: