Tuesday, October 11, 2011

Kumbukumbu ya mahafali ya Belo

Prosper Belo a.k.a Sabuni amekuwa mdau mkubwa wa blog hii. Mara kwa mara amekuwa akitoa maoni yake na hasa ninapomchokoza kwa mambo ya Yanga. Ni mnazi mkubwa wa Yanga. Belo ni mtaalamu wa IT alihitimu mwaka 2009 huko Arusha.Zaidi ya yote Belo ni shemeji yangu nimemuolea dada yake. Hivi sasa yuko pale Airport katika kampuni moja akicheck systems. Katika kupekua maktaba yangu nilikutana na picha hii. Kushoto ni mama mzazi wa Belo-Mama Mapunda na kulia ni shemeji yangu Mwamgeni alienda kumpongeza kaka yake Belo kwa kuhitimu masomo yake ya IT wakati ule akiwa Arusha sasa yuko Zanzibar kwenye mafunzo ya utalii na huduma za hotel.

Nikuulize Belo kwanini joho lenu lilikuwa na rangi nyeusi na zambarau? Na kwanini majoho mengi asilimia kubwa ya rangi ni nyeusi? Na kwanini hizo kamba zinazoning'inia kwenye kofia ya kisomi zimelalia mkono wa kushoto na zina maana gani? Wasomi mliovikwa majoho nipatieni majibu.

1 comment:

Belo said...

Nashukuru sana kwa kuweka hii picha,hii ni moja ya siku ya kukumbukwa katika maisha yangu.Shem hili la rangi za majoho sifahamu sababu ila ni utamaduni tulioiga kutoka kwa wazungu.Hizo kamba kabla hamjahitimu zinalazwa upande wa kulia ,mkisha hitimu mnazilaza upande wa kushoto