Monday, October 3, 2011

Ofisi za walimu

Na hilo ndilo jengo la utawala-Matombo Sekondari. Enzi yake ofisi ya Headmaster ilikuwa mkono wa kulia. Wakati nasoma nilibahatika kuongozwa na maheadmaster takribani wawili. Kajetan Banzi na Semindu (Siyo Semindu power). Nakumbuka demo ya gwaride alililokuwa akitoa Headmaster Semindu ilikuwa acha mchezo hadi mashavu yanatikisa huku mustache wake ukiruka ruka. Ndiyo, enzi hizo ualimu ulikuwa na thamani kubwa na cheo cha Headmaster ndiyo ilikuwa mwisho wa reli!. Hata watoto wao walikuwa wakiheshimika. Ah huyo mtoto wa mwalimu bwana! Sasa ualimu kwishine!

No comments: