Monday, October 3, 2011

Kutoka Matombo hadi Kisemvule


Tulizungumza sana tukikumbuka enzi zetu kule nyumbani Matombo. Mashindano ya sabasaba ambapo yeye alikuwa bingwa wa kukimbia mita 100 nafikiri ingekuwa kwa wenzetu hivi sasa angefananishwa na H.BOIT.Stori za 'solono' (kupiga mbizi) mtoni mfizigo hazikukosekana pia. Tuliwakumbuka wazee maarufu, walimu waliotufundisha hata, wanafunzi watukutu walevi wa kijijini waliokuwa wanawasumbua, sikukuu za kanisa hasa ekaristi kuzunguka kijiji cha Kiswira na hata wasichana watanashati waliotetemesha pale kijijini enzi hizo wengine hawapo tena nasi duniani.

No comments: