Monday, October 3, 2011

Shule yangu ya Msingi

Baada ya mazishi, nilipata fursa ya kutemebelea shule yangu ya Msingi Matombo iliyoanzishwa mwaka 1945 wakati huo ilikuwa ikijulikana kama Matombo Middle School. Niliingia hapo nikiwa darasa la tano. Mlango wa pili kutoka kushoto ndilo lililokuwa darasa langu 7B. Sasa inajulikana kwa jina la Shule ya Sekondari Matombo. Enzi zetu tulijifunza useremala katika shule hii . Tulipiga 'Brass Band' (mimi nilipuliza filimbi,ngoma ndogo na kubwa na wakati mwingine nikishika gongo-bandmaster!)katika shule hii, Niliwahi kuwa timekeeper katika shule hii kwani nilikuwa naishi karibu sana na shuleni lakini pia nilikuwa nafahamu kusoma saa. Tulicheza mpira shuleni hapa na kuanizsha klabu ya Kiswira mwaka 1971. Gwaride tulipiga kwenye uwanja unaoonekana hapo juu bila kusahau kuwa tulikuwa tunapata uji wakati wa mchana!

No comments: