Saturday, July 12, 2014

Tunakutana na wanasayansi wa IARI



 Siku ya pili ya ziara yetu, tarehe 8/7/2014. Tulitembelea 'Indian Agricultural Research Institute' (IARI). Taasisi hii ndiyo yenye dhamana ya utafiti wa kilimo (mazao) nchini India. Ni Taasisi yenye umri wa takaribani miaka zaidi ya 100. Taasisi hii pia inatoa shahada za uzamili(MSc) na Uzamifu (PhD) si kwa wahindi tu hata kwa mataifa mengine. Wanashughulika pia na usambazaji wa Teknolojia (Extension). Taasisi hii imefanya tafiti nyingi na mafanikio ni makubwa katika kutatua matatizo ya wakulima nchini India na kuboresha uzalishaji, kuongeza pato la taifa na kuinua maisha ya wakulima.Pichani tunapata maelezo ya muhtasari wa shughuli za Taasisi kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Taasisi hiyo.














No comments: