Tuesday, July 15, 2014

Utadhani Madaktari!






Maabara yana masharti yake. Sayansi ni kufuata taratibu bila ya hivyo mambo huharibika. Moja ya sharti ya kuingia kwenye maabara hii ni kuvaa makoti. Tulipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo India (IARI) tulipata fursa ya kutembelea kituo/maabara ya utafiti wa mimea katika mazingira ambayo siyo ya kawaida - kitaalamu inajulikana kama 'Phytophtoron.' Maabara hii ni kubwa na ya kisasa. Miundo mbinu iliyomo ndani ya maabara kwa kiasi kikubwa inaendeshwa kwa kompyuta. Hapa mimea inajaribiwa katika mazingira tofauti  kama vile hali ya joto,mwanga,maji na rutuba. Maabara hii hufanya kazi mwaka mzima. Mtafiti anapofanya jaribio lake katika maabara hii hakuna kusingizia kuwa jaribio halikuweza kuendelea kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa. Kwa sababu katika maabara hii kila kitu kiko ndani ya uwezo wa mtafiti. Kwa kufanya hivyo matokeo ya utafiti hupatikana katika muda uliopangwa.Ushirikiano kati ya watafiti, wahandisi na wafanyakazi wengine ni mkubwa katika maabara hii, kwani lengo ni moja na kufanya utafiti na kutoa matokeo haraka.

No comments: