Tuesday, July 8, 2014

Ziara mara moja


Prof. K.C.Bansal
Maeneo ya msukumo wa utafiti ya Taasisi
Dr. Mohamed Bahari- Kiongozi wa msafara
Bi. Yusta Katunzi kutoka kitengo cha usambazaji wa teknolojia za Kilimo
Watafiti wa National Bureau of Plant Genetic Resources
Mtafiti wa Kike wa NBPGR

Maelezo kutoka kwa Prof. Bansal kuhusu takwimu za nasaba za mimea ya mazao zinazotunzwa katika Taasisi

Mara baada ya kuwasili nchini India tulianza programu ya mafunzo siku hiyo hiyo kwa kutembelea  'National Bureau of Plant Genetic Resources.' Hii ni Taasisi ya Taifa ya Kutunza Nasaba za Mimea ya Mazao. Ni Taasisi kubwa yenye uwezo mkubwa katika raslimali. Watafiti mahiri na vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi. Nikilinganisha na kituo chetu cha Taifa kilichopo Arusha - National Plant Genetic Resource  Centre  pale TPRI bado tunasafiri ndefu ya kufikia hatua waliyofikia wenzetu  Wahindi. Hivyo inatubidi kuanza kuimarisha kituo chetu  na hapa tumejifunza mengi ya kuweza kuboresha kituo chetu cha Arusha tukiweka utaratibu mzuri wa kushirikiana na Taasisi hii.














No comments: