Wednesday, July 16, 2014

Uzalishaji kwenye udongo wenye chumvichumvi india


CSSRI ni kifupi cha 'Central Soil Salinity Research Institute.' Hii ni Taasisi ya Utafiti wa Udongo wenye chumvi nchini India. Taasisi hii imepewa kazi ya kutoa ufumbuzi wa uzalishaji kwa maeneo yenye udongo wa chumvi chumvi ambao unasababisha uzalishaji mdogo wa mazao au kutozalisha kabisa hivyo kuwafanya wakazi wa maeneo hayo kuishi kwa kubangaiza. Tatizo hili nchini India ni kubwa.

Kama mnavyofahamu nchi ya India ni Penisular. Karibu sehemu kubwa imezungukwa na maji tena ya bahari hivyo chumvi imeathiri sehemu kubwa ya ardhi ya India. Kwa kuona tatizo hilo Serikali ya India imeunda CSSRI. Taasisi hiyo imeshafanya tathmini ya maeneo yaliyoathirika na kufanya tafiti mbalimbali za udongo  na kutoa teknolojia mbalimbali za kuboresha uzalishaji kwa mazao,mifugo na mifumo mingine ya kilimo. Moja ya teknolojia hizo ni uzalishaji wa aina za mbegu za mpunga zinazostahimili chumvichumvi .Aina hizo ni  CSR 27, CSR 30 na CSR 36.

Tatizo hili hata hapa Tanzania ni kubwa, kwa sehemu ambazo zinafaa kuzalisha mpunga lakini kutokana na chumvi mpunga umeshindwa kustawi. Utafiti wa kutatua tatizo hili unaendelea katika Kituo chetu cha Utafiti cha KATRIN- Ifakara. Kuna haja ya kuanzisha mashirikiano ya kitaalamu kwa pande zote mbili kuweza kufanya tafiti za pamoja za kupambana na tatizo hili na kuweza kuwasaidia wakulima wetu ili waweze kuzalisha mpunga kwenye maeneo yenye chumvi.

No comments: