Saturday, July 12, 2014

Utafiti wa kweli wa ' Post harvest Technology' - IARI















Utafiti wa 'Post Harvest Technologies' unafanyika kwenye  taasisi ya Utafiti wa Kilimo India (IARI). Hapo mazao yanaongezewa thamani kwa  kutengeneza bidhaa nyingi zaidi kutokana na zao moja. Kwa mfano hapo tuliona jinsi mpunga (mchele) unavyoongezewa thamani na kutoa vitafunwa ambavyo vinachanganywa na viungo. Utengenezaji wa vinywaji baridi (juices) kutokana na matunda mbalimbali. Uhifadhi wa nyanya n.k. Aina hii ya utafiti haujafanyiwa kazi sana nyumbani Tanzania na Taasisi zetu za utafiti hivyo inabidi kujenga uwezo wa watafiti na kuzipatia taasisi zetu zana za kufanyia utafiti huo. Utafiti hauna faida kama hauwezi kutufikisha kwenye maendeleo ndiyo maana tunasema 'Research and Development.' Kinachotakiwa kufanya kwa sasa ni kujenga uwezo wa watafiti na kuimarisha miundo mbinu ya utafiti.

No comments: