Tuesday, September 3, 2013

Furaha ya kutembelewa

Dada Joyce anaecheka akiwa na familia na rafiki zangu kijijini Kisemvule
Watanzania tuna utamaduni mzuri wa kutembeleana. Hivi karibuni familia yangu ilibahatika kutembelewa na dada Joyce Eston Mashauri (Mama Lupi) na mwanaye Lupi. Dada Joyce alikuwa rafiki kipenzi wa marehemu mama yangu wakati tulipokuwa tukiishi pale Magomeni Qtrs.Kwa kweli tulishi kwa ushirikiano mkubwa. Hivi sasa dada Joyce anaishi Mbezi Makabe jijini Dar.

No comments: