Thursday, June 28, 2012

TTRI katika kutokomeza Mbung'o

'Tsetse and Trypanasomiasis Research Institute' (TTRI) kilichoko mkoani Tanga ni kituo mahiri kinachojishughulisha na utafiti wa mbung'o na ndorobo. Kituo hiki chenye historia tangu mwaka 1971 kilipoanza kama Mradi wa Utafiti wa Mbung'o kimefanya makubwa katika kutokomeza mbung'o ambao husababisha ugonjwa hatari wa malale kwa binadamu na ndigana kwa wanyama. Mwaka 1997 walifanikiwa kutokomeza wadudu hao visiwani Zanzibar kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ijulikanayo kwa jina la International Atomic Agency (IAEA) kwa kutumia teknolojia ya 'Sterile Insect Technique' (SIT). (Pichani Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Furaha Mramba akitoa maelezo kwa timu ya ufuatiliaji na Tathmini kwa shuguli za Utafiti chini ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo -ASDP)
Hiki ni moja ya kifaa kinachotumiwa katika utafiti wa ndorobo ni pekee Afrika Mashariki na ya Kati.
Mitego ya mbung'o

No comments: