Thursday, June 28, 2012

Utafiti wa ngozi

Ukielezwa thamani ya ngozi na jinsi walanguzi wanavyowaibia wafugaji unaweza kulia. Watafiti wa kituo cha Utafiti wa Mifugo Tanga wameanza kutafiti jinsi ya kuboresha thamani ya ngozi kuanzia uchinjaji wa wanyama, uchunaji ngozi, utayarishaji ngozi, utunzaji na hata kuitafutia masoko. Mtafiti Masakia kutoka kituo hicho anaeleza kuwa kipande kidogo cha ngozi ya mbuzi kwa kawaida huko vijijini mkoani Tanga huuzwa kwa shilingi 300 lakini kikiandaliwa vizuri kinaweza kuuzwa kwa shilingi 15,000. Hivyo hivyo kwa ngozi ya ng'ombe ambayo wafugaji huuza kipande kwa kiasi cha shilingi 2,000 hadi 3,000 lakini walanguzi hukiuza hadi shilingi 150,000/- kwa ukubwa unaofanana.Utafiti unaoendeshwa katika wilaya ya Handeni utawawezesha wafugaji kuboresha ngozi na kuboresha vipato vyao. Ngozi ni mali!
(Pichani Mtafiti Bariki Masakia akitoa maelezo ya utafiti wake wa kuongeza thamani ya ngozi).
Mwanakikundi na fundi (Bw. Saidi) wa bidhaa za ngozi mjini Handeni akionyesha mkanda aliotengeneza kutokana na ngozi ya mbuzi iliyoongezewa thamani.
Mwanakikundi ambaye ni fundi akionyesha cherehani yake anayoitumia kwa kushona bidhaa zinazotokana na ngozi.Hapa ndipo Halamashauri ya Handeni inapoweza kutoa mchango wake mkubwa kwa vikundi hivi kwa kuwapatia mashine bora na mtaji wa kupanua shughuli wananchi wanaojihusisha na utengenezaji wa bidhaa zinazotokana na ngozi hivyo kuwaongezea kipato chao na kipato cha Halmashauri kutokana na makusanyo ya kodi.

No comments: