Friday, August 24, 2012

Bi.Christina Mndeme na Kilimo

Nikiwa kwenye viwanja vya Temi jijini Arusha kwenye maonyesho ya kilimo nilibahatika kukutana na Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mh. Bi.Christina Mndeme.Nilifahamu mengi kutoka kwake. Kwanza anaifahamu vizuri wilaya yake na shughuli za uzalishaji wa kilimo zinazofanyika wilayani.Amenieleza jinsi wilaya inavyoshirikiana na vituo vya utafiti wa kilimo kama vile Mlingano kwa masuala ya ramani na matumizi ya mbolea, Selian katika uzalishaji wa ngano na shayiri na kushauri kuwa watafiti wasambaze matokeo ya utafiti kwa wadau.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mh. Bi Christina Mndeme
Kijishamba cha maonyesho ya zao la mahindi kwenye banda la Halmashauri ya Hanang
Bi Christina Mndeme akinunua bidhaa za asili kwenye banda la Hanang.

No comments: