Saturday, August 11, 2012
Katibu Mkuu WKCU - Nanenane Arusha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika (WKCU) Bw. Mohamed Muya (mwenye T-SHIRT nyeusi na cap nyeusi)akipata maelezo ya kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa vitengo mbalimbali kwenye banda la Wizara kwenye viwanja vya Temi -Arusha wakati wa maonyesho ya Nanenane 2012.Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kaskazini Dkt. Lucas Mboyi Mugendi akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu kuhusu teknolojia za kilimo zilizobuniwa na watafiti mbalimbali mbali hasa wa kanda hiyo.
Hapa Katibu Mkuu anapata maelezo kuhusu ruzuku ya pembejeo kushoto kwake (Mwenye cap nyeupe)Mratibu wa Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kaskazini Bw. Charles Lyamuchai akisikiliza kwa makini.
Katibu mkuu anapata maelezo ya kupambana na visumbufu vya mimea hasa nzige,viwavi jeshi na ndege aina ya 'queleaquelea'
Na hapa Katibu mkuu anapata maelezo matumizi ya aina mbalimbali za mbolea kwenye zao la mahindi na hasa matumizi ya mbolea za kupandia za Minjingu mazao na DAP.
Katibu Mkuu Mawasiliano wakati wote akiwa amezungukwa na maafisa waandamizi wa kilimo wa Kanda ya Kaskazini akiwemo Afisa Kiungo wa Kanda (Mwenye koti jeusi) Bw. Jeremiah Sembosi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment