Friday, June 13, 2014

Balaa ya 'Morogoro Road' tarehe 11/06/2014 Jumatano

Wengine ilibidi kusafiri kwa bodaboda ili wawahi wanakokwenda

Malori kwa kweli ni tatizo


bus la abood nalo ndani ya msongamno

huku BM na kule lori la cocacola kazi  kwelikweli

Hapa ni Kibaha mizani

Du bonge la mzigo!

Na hili nalo limebeba mbao
Jamani niwaishe - ndivyo anavyosema mwanadada aliyejuu ya bodaboda

wanafunzi wakitembea kwa miguu  kando ya barabara kwa kukosa usafiri





Hiki ndicho kilichotokea  tarehe 11/06/2014 barabara ya Morogoro. Ajali iliyotokea Kibamba ilisababisha msongamano mkubwa wa magari kutoka Mbezi hadi Kibaha. Nilifika Mbezi kwenye pacha ya barabara kwenda Kinyerezi muda wa saa 12.30 asubuhi, tulifika Morogoro saa 6.30 mchana! Abiria wengi wanaotumia barabara hiyo wanasema sikuhizi ni jambo la kawaida kabisa kukuta msongamano wa aina hiyo. Magari ni mengi sana hasa magari makubwa ya mizigo. Magari haya mengi hupata ajali yakiwa safarini na huchukua muda mrefu kuyaondoa barabarani ndipo hapo msongamano unapoanza. Mizani nayo ni chanzo cha msongamano, magari mabovu nayo pia ni sababu. Kuua mashirika ya reli hapa nchini ni sababu kubwa sana kwani kwa sasa mizigo mingi husafirishwa kwa njia ya barabara. Mwito wangu kwa serikali ni kufufua mashirika ya Reli  ya TAZARA na Tanzania Railway Authority achana na Limited. Reli hizi kwa silimia kubwa ziendeshwe na serikali yenyewe. Njia hizi kuu za usafirishaji ni muhimu kwa uchumi wa nchi yetu.

No comments: