Monday, June 16, 2014

Ulaji 'KOMBE' unahitaji uzoefu

'KOMBE' uwanjani


Wakati wa kula kombe mnaimbiwa huku shuka au kanga ikirushwa juu ya vichwa vyenu ikiwataka walaji kutunza fedha

'KOMBE' ni chakula maalumu anachoandaliwa Bw. harusi pamoja na wapambe wake kukila baada ya kufunga ndoa. Lakini pia, Bi harusi hula baada ya kutengewa mahsusi na mumewe. Hivi majuzi nilifanikiwa kupenyeza katika timu ya walaji kombe kwenye harusi ya mpwa wangu Sophy Mluge iliyofanyika maeneo ya Tumbaku kule Morogoro.Kuna mtaalamu aliyenishinda,  kwani wakati nasubiri kukata paja la kuku kuna ustaadhi aliwahi na kuliweka kwenye himaya ya mkono wa kushoto huku wa kulia ukiendelea kupapasa  samaki mkubwa aliyekaangwa. Niliambulia tambi na kipande cha samaki. Ama kweli ulaji wa 'KOMBE' unahitaji uzoefu!

No comments: