Friday, June 13, 2014

Biashara ya gesi kama simu ya mkononi





Biashara ya gesi ya matumizi ya nyumbani imeanza kupamba moto jijini Dar. Karibu sehemu nyingi zimefunguliwa  huduma za kupata gesi hiyo. Makampuni ya kusambaza gesi sasa yameongezeka. Ninayoyafahamu mimi ni Lake, Mihan, Oryx yanaleta  ni ushindani mkubwa katika sekta hiyo. Hali hii ikiendelea ukataji miti kwa ajili matumizi ya mkaa yatapungua kwa kiasi kikubwa. Bei ya gesi nayo itapungua. Jambo hili linabidi kuangaliwa kisera ili kupunguza bei ya gesi pamoja na majiko yake ili walio wengi waweze kumudu kutumia gesi hivyo kunusuru mazingira.

No comments: