Tuesday, June 3, 2014
Mkutano wa Wazazi Shule ya Sekondari Vikindu
Tarehe 31/05/2014 siku ya Jumamosi ulifanyika mkutano wa wazazi Shule ya Sekondari Vikindu iliyoko Wialya ya Mkuranga mkoa wa Pwani ulioitishwa na Bodi ya Shule ili kujadili Maendeleo ya Shule hiyo yakiwemo masuala ya miundo mbinu, taaluma na nidhamu. Kitaaluma shule hiyo haijafanya vizuri kwenye mtihani wa Kidato cha Nnne 2013 kwani asilimia 61 ya wanafunzi waliofanya mtihani huo walipata daraja la 0. Hata hivyo shule hiyo ina mazingira mazuri na walimu wenye ari wakiongozwa na mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bw. Humphrey Mapunjo. Tayari maabara ya sayansi yanakaribia kukamilika kwa kuweka vifaa vya maabara. Katika mkutano huo wazazi waliazimia kutoa michango ya ziada ili kuwawezesha walimu kutoa mafunzo wakati wa ziada pia kuboresha mazingira ya shule kwa kuongeza matundu 20 zaidi ili kufikia 40 ili yaweze kutumiwa na wanafunzi. Kwa sasa shule hiyo hutoa huduma ya uji wenye virutubisho bora ili kuweza wanafunzi kuendelea na masomo bila kuchoka ingawa baadhi ya wazazi wamekuwa wagumu kuchangia kiasi kidogo cha fedha sawa na Tshs 50/= kwa kikombe cha nusu lita kwa siku.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment