Monday, June 9, 2014

Tuwafikishe wakulima wetu kwenye mazingira haya

Kwa mazingira haya mkulima ataheshimika, kilimo kitaheshimika na kwa kweli tutauaga umasikini. Inawezekana lakini hatujitambui. Mimi napenda kuishi mazingira kama haya. Sihitaji geti la bati au chuma, miti inatosha, sihitaji ukuta wa zege uzio wa miti hai inatosha na inapendeza. Nahitaji kuwa na maji, mifugo michache, matunda, mazao ya chakula na biashara pia sehemu ya michezo ya kujenga afya yangu na familia yangu. Wewe je? Hili ni lengo la RIPAT (Rural Initiatives for Participatory Agricultural Transformation)- Jitihahada Shirikishi za Kuleta Mageuzi ya Kilimo Vijijini. Lengo la RIPAT ni kuona kaya bora yenye mwelekeo wa picha hii.

No comments: