Thursday, August 21, 2008

Huree nimefikisha Post 100!

Namshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema, akili timamu na fursa ya kutosha ya kuweza kuingiza post 100 hadi sasa. Hili lilikuwa ni lengo langu la mwaka 2008. Miaka iliyotangulia zikuweza kufikisha hata post 25 kwa mwaka. Lakini mwaka huu nimeweza, nimevunja rekodi yangu mwenyewe.
Lakini kuna sababu nyingi zilizonifanya niweze kuingiza post nyingi mwaka huu. Mwaka huu nilipata fursa ya kusafiri sehemu mbalimbali nchini kikazi. Nimehudhuria mikutano, semina na warsha nyingi ambazo zimeniwezesha kukusanya niliyoyaona yanafaa kuwepo kwenye blog hii. Safari yangu Mbeya kwenye maonyesho ya Nane Nane nimejifunza mengi na nimeandika mengi kwenye blog hii kuhusu Nane Nane Mbeya.

Safari za kwenye Kanda kwa ajili ya kutoa elimu kwa wadau kuhusu Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP) nayo imeniwezesha kukusanya habari kutoka Tabora, Arusha, Mbeya, Morogoro na Pwani.
Usafiri wa daladala nao umeniwezesha kupitia na kuona mengi ya jiji hili la Dar Es Salaam. Niliyoyasikia na kuyaona nimeyaning'iniza kwenye blog hii ingawa si yote.

Maisha yangu kijijini Vikindu-Kisemvule, ushiriki wangu katika shughuli za Parokia ya Kanisa Katoliki Vikindu pia ni hazina kubwa kwangu katika kufurisha blog hii. Naamini kuwa nitaweza kuingiza mengi kwenye blog hii kabla ya mwisho wa mwaka 2008 na iwapo nitapata camera habari zitaambatana na picha. Wateja wa Banzi wa Moro naomba maoni yenu

1 comment:

Belo said...

Hongera sana kwa kufikia lengo lako la post 100 ingawa ulikuwa umebanwa na kazi,ushauri wangu ni
1.Tafuta Digital Camera then uwe unapost habari na picha
2.Jaribu kuwasiliana na blog maarufu kama mjengwa,michuzi,bongo celebrity ili waweke link ya blog yako kwenye blog zao
3.Nakupongeza kwa kuweza kutoa habari za mikoa tofauti kuhusu maendeleo na habari za nyanja mbalimbali kama kilimo,siasa,michezo