Baadhi yetu tumeshakula chocolate au kunywa kinywaji cha milo. Lakini je,tunafahamu kuwa hivyo vyote hutengenezwa kutokana na zao la kakao (cocoa). Hapa Tanzania kilimo cha kakao kimeshamiri sana wilayani Kyela mkoani Mbeya. Lakini nina matumaini kuwa utafiti wa kutosha ukifanyika kwenye ikolojia inayofanana na Kyela kokoa inaweza kustawishwa sehemu nyingi na kuwaingizia kipato wakulima wetu. Nchi ya Ghana hutegemea sana zao la Kakao katika pato la Taifa. Tuwe na mikakati ya kupanua kilimo cha Kakao katika nchi yetu.
No comments:
Post a Comment