Saturday, October 25, 2014

Misa ya Mavuno Jumuiya ya Mt. Vincent Parokia ya Vikindu - 25/10/2014





Leo 25/10/2014 asubuhi, Padri Jinu wa Parokia ya Vikindu aliendesha  ibada ya misa takatifu ya mavuno iliyodhinishwa kwenye Jumuiya  ya Mt. Vincent. Kwenye mahubiri yake alisema kuwa, mara nyingi binadamu tunamsahau MUNGU. Tunapofanikiwa katika maisha yetu tunafikiri ni kwa sababu ya akili zetu au juhudi zetu binafsi. MUNGU TUNAMUWEKA KANDO. Tujiulize katika maisha yetu, hivi hatuna chochote cha kumwambia MUNGU ASANTE? Na hii ndiyo maana ya MAVUNO ni kutoa SHUKRANI KWA MUNGU. Tumsifu YESU KRISTU.

No comments: