Friday, March 7, 2014

Wakulima wa mpunga - Lower Moshi mafunzoni manunuzi ya mbegu bora za mpunga

Washiriki wa mafunzo ya ununuzi wa mbegu bora za Mpunga wakiwa na wawezeshaji chuoni KATC-Moshi
Baadhi ya wadau waliohudhuria mafunzo ya manunuzi ya mbegu za mpunga chuoni KATC mwezi Februari 2014
Wakijadiliana jinsi ya kutumia mbegu ya mpunga SARO 5 waliyoipata kwenye mafunzo.
Washiriki wa mafunzo wakielekea kwenye bwalo la chakula
Wakulima wakiwa katika majadiliano
Wakulima wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa muwezeshaji wa mafunzo

Mkulima akiwasilisha kazi ya kikundi
Afisa Ugani wa wilaya ya Moshi (kushoto) na mwezeshaji Mama Ruth Kamala wakelezana jambo kwenye mafunzo hayo.
Mwezi Februari 2014  Mradi wa Kuongeza Uzalishaji na Tija  katika Kilimo Mashariki mwa Afrika (EAAPP) uliendesha mafunzo kwa wakulima na wadau  15 wa mpunga wa kutoka Lower Moshi, mkoa wa Kilimanjaro. Madhumuni ya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wakulima hao pamoja na wauza pembejeo hasa wa mbegu za mpunga  kununua mbegu bora za mpunga na ujuzi wa kufanya mapatano katika manunuzi.

No comments: