Saturday, March 22, 2014

Post yangu ya kwanza nikiwa Matombo

Jana tarehe 21/03/2014 niliwasili kijijini kwangu Matombo, Morogoro ni siku ya Ijumaa. Nilipata bahati kushiriki  Njia ya Msalaba ndani ya kanisa hilo nilimobatizwa, kupata Komunio ya Kwanza na Kipaimara. Waumini wachche waliohudhuria wengi walikuwa ni wanawake kuliko wanaume. Hali hii inafanana sana na Parokia yangu ya Vikindu Jimbo Kuu la Dar Es Salaam. Wanawake wengi wanatenga muda wao  kushiriki ibada  sisi wanaume tuko 'busy'. Namshukuru Mungu hii ni post yangu ya kwanza nikiwa Matombo baada ya miaka mingi sehemu hii ya Tanzania sasa imepata umeme tangu mwaka 2013 mambo haya sasa yanawezekana.