Thursday, March 6, 2014

Bustani barabarani Mtoni Mtongani Dar Es Salaam

Kila nikipita barabara hii ya Mtoni  mtongani  kujiunga na barabara ya Kilwa kuelekea Mbagala Rangi tatu navutiwa na bustani hiyo iliyo kando ya nyumba hiyo hapo juu. Bustani ni ndogo lakini ni nzuri kwa kuwa inatunzwa. Huwa najiuliza kwanini wenye nyumba nyingine kando ya barabara hiyo wasiige mfano wa bustani hii kando ya nyumba zao? Kama wangefanya hivyo kwa kweli barabara  hii ingevutia na ingekuwa mfano wa kuigwa jijini Dar.

No comments: