Monday, March 31, 2014

Sehemu ya 'Kupolisi' kanisani Matombo

Nilipokuwa mdogo nilimsikia Babu yangu Mzee Mwl. Ephrem  Kobelo a.k.a Mzee  Vibaya akinieleza kuwa sehemu hiyo iliyotengwa kanisani ni kwa ajili ya 'kupolisi'. Mara nyingi nilimuona Padri akishamaliza kusoma Injili hupanda ndani ya chombo hicho na kuanza kuhubiri. Siku hizi mapdri hawakitumii tena. Akiwa ndani ya chombo hicho waumini waliweza kumuona barabara naye kuwaona waumini. Na ikumbukwe kuwa wakati huo kulikuwa hakuna vipaaza sauti. Pengine sasa hatuhitaji tena chombo hiki kwani tuna vipaaza sauti. Tutawaeleza wajukuu wetu kuwa hiyo ni sehemu ya kupolisi. Huenda Paroko wa Matombo wa sasa Fr. Kobelo atakitumia chombo hiki wakati wa sherehe ya Pasaka mwaka 2014!

No comments: