Monday, March 31, 2014

Darini kwa waimbaji kanisani Matombo

Nilibahatika kusali njia ya msalaba  Ijumaa ya tarehe 21/04/2014 kanisani Matombo. Nilipogeuka nyuma na kutazama juu nikaona sehemu ya darini walipokuwa wakikaa waimbaji na kuimba Noel ! Noel !ajaye Mtu MUNGU!  au Mkristu Miye niko salama shetani wee usinijie......Hakika siku zinapita kwa kasi na mabadiliko ni mengi. Wakati huo kinanda kilikuwa kikiporomoshwa na Babu marehemu Mwl. Paul Lugonzo au Marehemu Mwl. Isdori Baggo.Mungu awalaze mahali pema peponi AMINA. Siku hizi waimbaji wanaimba wakiwa mbele kanisani na huku kinanda kikiwa chini!

No comments: