Saturday, March 22, 2014

Matombo maarufu kwa mazao ya tropiki

Hapa ni Matombo, kijijini Kiswira. Mazao ya aina mbalimbali ya kitropiki yanastawi kama inavyonekana pichani. Machungwa,migomba,minazi,muhogo,mashelisheli mananasi na maembe. Ugonjwa wa mnyauo unaoathiri migomba haujaingia sehemu hii. Kuna umuhimu wa kuweka mikakati ya uzalishaji wa zao la ndizi hapa Matombo kwa ajili ya chakula na kuongeza kipato cha wananchi wa sehemu hii  na kuimarisha pato la taifa. Watafiti wa Kilimo wanatakiwa kuongeza juhudi ya kutathmini sehemu hii na kuishauri serikali  jinsi ya kuwaendeleza wakulima wa eneo hili wakishirikiana na wagani.

No comments: